WANAOTUFUNDISHA KUTUMIA KONDOMU, WANATUFUNDISHA KUUA!
Mjadala juu ya matumizi ya kondomu umepamba moto na tumeshuhudia wajasiriamali wa kondomu wakiongezeka, aina za kondomu zikiongezeka tunaambiwa kuna kondomu zenye betri (Vibrating kondoms), kondomu zenye harufu mbalimbali! mfano harufu ya chungwa, embe, na nyinginezo nyingi haya ni maajabu ya Mussa!
Katika makala zilizopita za gazeti hili tumeshuhudia watu wanaotetea kondomu wakijenga hoja zisizo na ukweli wowote na kubaki wakipotosha umma! Hii ni hatari kwani upotofu unasambaa kama ilivyo kwa maambikizi ya ukimwi!
Kabla ya kuanza ya kutoa hoja labda tuangalie ni wapi ndugu zetu wamepotoka!
Mwanafalsafa wa siku nyingi Permanides anatuasa juu ya ukweli anasema watu wanachanganya kati ya ukweli kadri unavyojitokeza kwao-relative truth na ukweli halisi-objective truth anasema ni vizuri kuangalia kitu kama kilivyo na si-vinginevyo!, na hii ilimfanya mwanafalsafa Plato kuugawa ulimwengu katika makundi mawili,yaani ulimwengu wa busara na akili-intelligible world na ulimwengu wa mwonekano-sensible world na kadiri ya Plato wale wenye busara na fikara sahii wapo kwenye ulimwengu wa ukweli na wale wenye vionjo wapo kwenye ulimwengu wa maoni/maono!
Kwa hiyo wale wote wanaosema wanatoa maoni yao wapo kwenye ulimwengu wao wa VIONJO!
Labda tuangalie ukweli na uhalisia wa kondomu,Mosi azma ya awali ya kutengeneza kondomu haikuwa kuzuia ukimwi!
Pili mpaka sasa hakuna uthibitisho wowote uliotolewa na mwanasayansi ama taasisi yoyote kuhusu uwezo wa kondomu kuzuia ukimwi kwa 100%.
Tatu kama vitabu vyetu vitakatifu vinatuambia tusizini na kondomu inatuambia tuzini kwa kutumia silaha huku ni kuhalisha dhambi!
Nne falsafa ya kondomu kama inavyoendeshwa na wajasiriamali wa kondomu ni ya mauaji na kimsingi kondomu inafanya kazi kubwa mbili,moja kondomu inawasawishi watu wafanye ngono mfano picha nyingi sana zinazowekwa kwenye pakiti ya kondomu ni zile za ponografia na mengine niliyoyaeleza hapo juu ni wazi yanachochea ngono na tukumbuke sehemu wanazouza bidhaa hii wanaingia watu wa rika zote watoto,vijana na wazee kwa hiyo kuwaoshesha watoto ,vijana na wengine picha hizi ni kuwashawishi wafanye ngono na hili ni kinyume na sera za SERIKALI! Pili kupoteza pesa nyingi katika matangazo yanayosawishi matumizi ya kondomu na si-kuacha kufanya ngono hii ni dalili ya mauaji maana yake tunawashawishi watu waanze na C badala ya A au B.
Mfano Watu wengine wamefikia mpaka hatua za kubeza kampeni za SUBIRI AU TOSHEKA NAYE na wengine kuhusisha kondomu na kitubio hawa ni wauwaji wakubwa!
Na cha kushangaza utakuta watu hao labda walikuwa ni viongozi wa dini kwa miaka mingi iliyopita.
Lakini watu wanapata mashaka na watu hawa mosi kwa kadri ya taratibu za dini zao tunaambiwa watu hawa wanauishi useja je watu hawa waliishi maagizo haya? Kama waliishi maagizo haya je mbona wanawafundisha watu watumie kondomu? Na kama walishindwa kwa nini wanawashawishi watu wafuate maanguko yao?
Ukiangalia kwa makini maswali hayo utagundua watu hao utagundua hawana tofauti na wale aliowazungumzia mwanafalasafa Permanides na Plato yaani watu wa vionjo!
Lakini pili watu hao wanaolingalisha kondomu na kitubio utagundua kuwa wameshindwa kuelewa zana ya “mkosefu kusamehewa na aliyekosewa kusamehe” hii ni maana halisi ya KITUBIO kwa maana kitubio kinalenga katika kurudisha mahusiano yaliyopotea,lakini twaweza kusema kuwa watu hawa si-watu wanaowasamehe wenzao wala wao hawapedi kusamehewa na mara nyingi watu hawa huwa viburi wa upatanisho!
Lakini kundi lingine ni hawa wananchi wa kawaida ambao wao wamekuwa wahanga wa tatizo hili,kimsingi hawa wanapata wakati mgumu sana kwani wakati serikali ikiubili juu ya matumizi ya kondomu taasisi za dini zinahubiri juu ya maagizo ya kuacha kuzini na kutotumia kondomu!
Wanaotumia kondomu kwa maana ya kushindwa kujizuia kufanya ngono wameshindwa pia kufuata maagizo ya muumba wao.
Ukiangalia uumbaji wa dunia utaona mungu aliumbwa vitu vyote na na baadaye akasema na sasa tumuumbe mtawala wa hivi vyote wanyama, ndege, mimea, ardhi nk soma Mwa. 1:26-28 “Mungu akasema na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale samaki wa baharini na ndege wa angani na wanyama na nchi yote pia na kila kitambaacho juu ya nchi.Mungu akaumba mtu kwa mfano wake kwa mfano wa Mungu alimwumba mwanaume na mwanamke aliwaumba.Mungu akawabariki, mungu akawaambia zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha, mkawatawale samaki wa wa baharini na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi”
Maneno tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, mwanaume, mwanamke, zaeni, ni maneno yanahitaji tafakari ya kina na utagundua binadamu kapewa mamlaka ya kutawala yote hata uzinzi!
Mazingira ya binadamu wa kwanza yaani Adamu na Eva ni yaleyale mfano wakati wale waliambiwa wasile matunda ya MTI WA UZIMA Mwa.2:15-17 sisi leo tunambiwa TUSIZINI na tumeshuhudia kwenye maandiko matakatifu madhara ya kukiuka maadili.
Matatizo mengi anayoyapata binadamu wa leo UKIMWI, RUSHWA, UMASIKINI, UHALIFU, ni matokeo ya kukiuka maadilI matakatifu.
Uongo juu ya uwezo wa kondomu kuzuia maambukizo ya ukimwi unafichuliwa katika taarifa za NACP, TACAIDS, mfano pamoja na kuongezeka kwa usambazaji na matumizi ya kondomu bado maambukizi yanaongezeka!
Binafsi naona kufundisha watu kutumia kondomu ni sawa tu na kuwafundisha watu namwa ya kuua! Mfano wanaofanya ngono wakiwa na virusi vya ukimwi kwa kutumia kondomu ni kuwafundisha watu kuua!!
Ni nani kwenye tendo la ndoa ata chukua kondomu ingine ili-hali ile aliyoivaa imetoboka au imevuka? Utajuaje kama kondomu imetoboka wakati wewe upo kwenye mshindo? Huku si kuwafundisha watu waue?
Kusema kondomu ni silaha ni kutuongopea! Na ni ubabaishaji mkubwa! Watu wananunua kondomu lakini pindi wanapoona tupu za wenzi wao kondomu ina-wekwa pembeni na watu wanaanza kufanza tendo la ndoa! Mwishoe wanaambukizana ukimwi!
Wataalamu wa saikolojia wasema maumbo ya binadamu yana nguvu kuliko kondomu na tendo la ngono lina nguvu kuliko kondomu hivyo utagundua kondomu si silaha bali UPOTOSHAJI TU!
Kamwe hatuwezi kutetea uhai,kuwa wema,kutenda haki, kumheshimu mungu kwa kutumia kondomu
Suala la kutotumia kondomu ama kuacha kufanya ngono/kuwa mwaminifu kwa mwenza wako kwa wale waliooa haliitaji MAJADILIANO/UTAMADUNISHO!
Hatuwezi kuheshimu uhai wa mtu kwa kuacha maadili ya Mungu yateketee! Tusiipake dhambi manukato dhambi ni dhambi tu! Kondomu haina uwezo wa kubadilisha dhambi kuwa tendo takatifu haiwezekani!
Kama tunataka kuheshimu uhai tuanze kuhubiri juu ya kuacha kufanya ngono kwa wale ambao hawajaoa kwani hakuna ugonjwa wowote unaosabibishwa na kutokufanya ngono! Pili tuhubiri juu ya uaminifu kwa wale wenye ndoa zao! Tatu tuhubiri juu ya kuheshimu maadili ya dini zetu.
Tuache ujasiriamali wa kondomu tutafute bidhaa nyingine za kuuza si kondomu haifai kuuzwa wala haiuziki!
Tukumbuke ya kuwa mafundisho ya vitabu vitakatifu yanasema TUSIUE wala TUSIZINI.
Na usanii wa Kufundisha watu kutumia kondomu kwa kigezo cha kuzuia ukimwi ni kuwafundisha watu kuua!
Ndimi
KILLIAN E. NANGO
P.O.BOX 9192
DAR ES SALAAM
Emaili:Killijunior@yahoo.com
“Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa PILI,taaluma ya Uhasibu katika Chuo cha usimamizi wa Fedha IFM-Dar Es Salaam.Msomaji makini wa Tanzania Daima Jumapili,na pia ni Mwanaharakati wa YUNA na TYVA”
Monday, March 19, 2007
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment